Byteq Plots Company Ltd ni kampuni ya daraja la juu inayomiliki, kupima na kuendeleza miradi ya viwanja vyenye hati miliki nchini kote.
Tangu kuanzishwa kwetu, Byteq Plots Company Ltd imesimama kama daraja imara la uaminifu kati ya mwekezaji na ardhi halali. Tunaelewa kuwa ununuzi wa ardhi sio tu matumizi ya pesa, bali ni msingi wa urithi na maendeleo ya kizazi chako.
Tukiwa na makao makuu yetu jijini Dar es Salaam (Kigamboni Ferry, Kibada Rd), tunajivunia timu ya wataalamu waliobobea katika sheria za ardhi, uratibu wa ramani, na usimamizi wa mali za kiwanja ambao wanahakikisha unapata hati yako bila ukiritimba.
"Umiliki wa ardhi iliyopimwa na yenye nyaraka halali ndio siri pekee ya utajiri usiotikisika duniani."
We Map Your Future
Hekari Zilizopimwa
Wateja Waliopo Ndani & Diaspora
Hati Miliki Zilizokabidhiwa
Kuwa taasisi nambari moja inayoaminika Afrika Mashariki katika kurahisisha umiliki wa ardhi salama na ujenzi wa makazi ya kisasa kupitia teknolojia na mifumo ya malipo yenye tija kwa kila tabaka la jamii.
Kutokomeza migogoro ya ardhi kwa kuwapatia wateja wetu ndani na nje ya nchi viwanja vilivyopimwa kwa vipimo vya kisasa vya setilaiti (GPS), vyenye miundombinu bora na hati miliki halali za kisheria kwa uwazi mkubwa.
Nguzo kuu tatu zinazotofautisha huduma zetu na soko la kawaida.
Kila mradi wetu unapitia taratibu zote za serikali na wizara ya ardhi. Hatuzi viwanja vyenye migogoro.
Tunauza viwanja vilivyopangwa kimkakati vikiwa na barabara, nishati ya umeme, na maji karibu.
Mifumo yetu ya malipo ya kidijitali na kidogo kidogo (awamu) inampa nafasi kila mtu kumiliki ardhi.